The Search
Shimo jeusi
Shimo jeusi ni jina la eneo katika anga-nje lenye mvutano kubwa, kiasi kwamba hata nuru haiwezi kutoka nje yake. Eneo hili lazungukwa na upeo usioonekana lakini mipaka ya upeo huo ni kama mstari ambao kila kitu kinachoupita hakiwezi kurudi tena kwa sababu kinavutwa mno na mvutano wa shimo jeusi. Eneo hili laitwa "jeusi" kwa sababu nuru yote inayofikia upeo huo inamezwa kabisa, hakuna inayorudishwa tena.
Wikipedia · CC BY-SA